Staa wa muziki wa pop kutoka Colombia, Shakira amefunguliwa mashtaka ya kukwepa kulipa kodi na serikali ya Uhispania ambapo anadaiwa kiasi cha $ Milioni 7.1.
Kiasi hicho cha pesa anachodaiwa ni kwa mwaka 2018, ambapo alikuwa akiishi Barcelona na nyota wa mpira wa miguu Gerard Pique, inaelezwa mrembo huyo alikuwa akikwepa kodi kwa nchi hiyo na badala yake alikuwa akitumia kampuni zinazomilikiwa na nchi zenye ushuru mdogo kulipa.