Mzee Donald mlemavu wa macho Mkoani Geita amlilia Mkuu wa Wilaya kumnusuru na makazi yasiyo na paa

Mzee Mmoja aliyefahamika kwa Jina la Donard Ndelela mwenye ulemavu wa Macho Mkazi wa Kijiji cha Kasota Kata ya Bugulula Halmashauri ya wilaya ya Geita Mkoani Geita amemwaga machozi mbele ya Mkuu wa wilaya ya Geita Hashim Komba akiomba msaada wa kununua turubai kwa ajili ya kufunika nyumba yake ambayo haijaezekwa wala kufunikwa na chochote.

Ndelela ametoa malalamiko hayo wakati akiwasilisha kero yake katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Kasota katika ziara ya Mkuu wa wilaya ya Geita Hashim Komba ambapo amesema kwa sasa analala kwenye nyumba ambayo haijaezekwa kwa chochote hivyo amemuomba Mkuu huyo wa Wilaya pamoja na wananchi kumchangia ili aweze kujisitili.

Baada ya mzee huyo kuwasilisha changamoto hiyo Mkuu wa wilaya ya Geita Hashim Komba amelazimika kuchangisha fedha kiasi cha 166,000 kwa baadhi ya wananchi na viongozi mbalimbali waliokuwepo katika mkutano huo ili kumsaidia mzee huyo na kuahidi kumjengea nyumba ambayo itakwenda kufunguliwa na mwenge wa uhuru 2024.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *