Mawakili Kenya, watangaza maandamano kupunga kauli ya Rais Ruto

Nchini Kenya, rais William Ruto ameendelea kukosolewa kwa kauli yake aliyoitoa akisema serikali yake haitaheshimu maamuzi ya Mahakama yatakayopinga miradi ya serikali yake, akiwashatumu baadhi ya Majaji kuwa wafisadi na wasiojali maslahi ya umma.

Jumanne ya wiki hii, Rais Ruto alisema kuwa baadhi ya majaji ambao hakuwataja majina wanashirikiana na wanasiasa wa upinzani pamoja na watu wenye nia ya kuzuia kuendelea kwa miradi ya serikali.

Kwa upande wake Jaji mkuu wa nchi hiyo Martha Koome, akijibu matamshi ya Rais Ruto, amesema kuwa kukiuka maamuzi ya mahakama ni kinyume na sheria kwa watumishi wa umma, huku akiwataka Majaji wa Mhakama kuendelea na kazi yao kwa mujibu wa sheria za nchi bila uoga na upendeleo.

Chama cha Mawakili nchini humo, kimetangaza maandamano ya nchi nzima, kupinga kauli ya Ruto wanayosema ni kuishambulia Mahakama na Majaji. Rais Ruto kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wa serikali Hussein Mohammed siku ya Jumatano, alikiri kuendelea na vita dhidi ya kile alichokitaja kama Mahakama kutoonekana kutochukuliwa hatua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *