Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

ARV inatumika kunenepesha kuku

Utafiti uliowasilishwa kwa Kamati ya Bunge nchini Uganda na Chuo cha Afya cha Makerere, hivi karibuni umebaini kuwa nguruwe waliolishwa ARVs(Dawa za kutuliza makali ya VVU) wanakua haraka na kunenepa lakini wanaugua mara kwa mara.

Mkaguzi Mkuu katika Mamlaka ya Kitaifa ya Dawa, Amos Atumanya, aliwaambia wabunge kwamba uchunguzi ulifanyika baada ya tahadhari kutoka kwa umma mnamo 2014, waligundua kuwa ARVs zimetolewa kwa nguruwe na kuku, lakini ripoti yake haikutangazwa.

Pia, ilithibitisha madai kwamba dawa hizo zilikuwa zikitumika kutibu ugonjwa wa Newcastle kwa kuku. Ambapo asilimia 33 ya tishu za kuku na 50 za nyama ya nguruwe zilizojaribiwa kutoka sokoni katika mji mkuu, Kampala, na mji wa kaskazini wa Lira, zilikuwa na mabaki ya ARVs.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *