Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma limesema hadi sasa mwili wa mwanamume aliyefahamika kwa jina moja la Amosi, anayedaiwa kumuua mpenzi wake kwa kumkata koromeo na kisu, hakuna ndugu aliyejitokeza kuutambua.

Mwanamume huyo anayejishughulisha na shughuli za ujenzi jijini Dodoma anadaiwa kumuua mpenzi wake Samira Mathiasi kwa kumkata koromeo kisha kujichoma kisu tumboni kwa kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Kamanda wa polisi, mkoa wa Dodoma, Martin Otieno, amesema mwili wa mwamume huyo umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Dodoma na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kuutambua mwili huo ili hatua nyingine ziendele.