Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Waliofanya mauaji ya mume na mke wahukumiwa kunyongwa

Mahakama kuu kanda ya Shinyanga imewahukumu kunyongwa hadi kufa washitakiwa wanne wa kesi ya mauji ya Bwana Mayara Ndelema na mkewe Nyamizi Mserengeti ambaao waliuwawa kwa kukatwa na mapanga na shoka sehemu mbalimbali za miili yao na kupekekea vifo vyao baada kuvamiwa usiku wakiwa wamelala na kufanyiwa ukatili huo Katika kijiji Masengwa halmashauri ya Shinyanga.

Shauri hilo namba 14 la mwaka 2022 linasikilizwa mbele ya Seif Kulita amesema ushahidi uliwasilishwa na upande wa mashitaka umethibitisha wazi bila kuacha shaka kwamba watuhumiwa wote wanne walishirikiana kwa pamoja kutenda kosa hilo Usiku wa wa tarehe 1 Juni 2019

Akisoma ushahidi amesema ushahidi umeweka wazi kuwa mshitakiwa no 1 Salawa Ndelema ambaye ni kaka wa marehemu Manyara Ndelema aliwakodisha watuhumiwa namba 2 3 na 4 ambao ni Mayala Maregele Shija Ngelanija maarufu kama tembo na Emanuel Manoni kufanya mauaji hayo kwa ujira wa shilingi milioni moja na laki mbili kwa pamoja kwa sababu alikuwa na mgogoro wa ardhi na mdogo wake huyo huku akimtuhumu shemeji yake marehemu Nyamizi Msengeti kuwa ni mchawi na amekuwa akimloga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *