Soko la Mbuyuni manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro limeteketea kwa moto na kuacha wafanyabiashara zaidi ya 2500 wakiwa hawajui la kufanya baada ya bidhaa zao zote kuteketea.
Moto huo ulioanza kuwaka majira ya saa sita usiku wa kuamkia leo na chanzo chake bado hakijajulikana,umesababisha hasara kubwa kwa wafanyabiashara hao ambao asilimia kubwa wanaendesha biashara kwa mikopo.