Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Watanzania 10 kusoma Romania

Serikali za Tanzania na Romania zimekubaliana kubadilishana wanafunzi katika vyuo vikuu vya nchi hizo mbili ili kuimarisha uhusiano katika sekta ya elimu.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mazungumzo ya ndani baina ya viongozi hao wawili, Rais Samia Suluhu Hassan amesema, Romania imekubali kutoa nafasi 10 za masomo kwa wanafunzi wa Tanzania kusoma katika vyuo mbalimbali vya nchi hiyo.

Rasi Samia pia amesema Tanzania itatoa nafasi kwa wanafunzi watano wa Romania kuja kusoma katika vyuo vikuu vya hapa nchini.

Mbali na kubadilishana wanafunzi, Romania na Tanzania pia zimekubaliana kushirikiana katika sekta ya uhifadhi wa misitu ambapo Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kitakuwa na jukumu la kutekeleza makubaliano hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *