
Mwanafunzi wa Sekondari ya Kilolo mkoani Iringa amefariki wengine 17 wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo baada ya kudaiwa kula chakula cha Msaada kilichotolewa kama Futari katika Msikiti wa Luganga
Afisa Afya wa Wilaya, Dkt. Fanuel Nyadwike amesema tayari Sampuli zimechukuliwa na kupelekwa kwa Mkemia Mkuu na kinachosubiriwa ni majibu , na wanachokifanya kwa sasa ni kuwapatia huduma wanafunzi ambao wamelazwa.
Tukio hilo limeibua maswali kuhusu msaada huo, na kuhoji ni watu wangapi walikula chakula na je, wote wamepata madhara?
Uongozi wa Shule haujapatikana kuongelea tukio hilo