Vifo vilivyotokana na maporomoko ya matope kutoka mlima Hanang’ mkoani Manyara, vimeongezeka na kufikia 69 baada ya miili minne kupatikana.
Msemaji Mkuu wa serikali, Mobhare Matinyi ameyasema hayo leo Jumatano wakati akizungumza na waandishi wa habari Wilayani Hanang, ambapo amesema vifo hivyo miwili ni wanawake na wengine wanaume.
Matinyi ameongeza kuwa awali kwenye ajali hiyo walikuwa majeruhi 117 ila wengine wamepata ruhusa, mmoja akafariki hivyo idadi yao hivi sasa imepungua na imebaki majeruhi 45.
Kwa upande wake Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson ameipongeza wizara ya afya kwa uharaka na kazi nzuri ya kuhudumia majeruhi hao, n kuwapongeza timu ya madakatri waliotoka mikoa ya jirani kufika mapema katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara kuongeza nguvu kwa ajili ya kuhudumia majeruhi.
04:56 PM
Jack JAMBO FMadmin