Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na Wananchi mkoani humo, limefanikiwa kumkamta Alex Msigwa (34) ambaye ni dereva Bajaji Mjini Iringa, kwa tuhuma za kuhusika kwenye matukio 15 ya ubakaji ambapo zaidi ya watoto 20 wenye umri wa kati ya miaka 6 mpaka 14 walibakwa kwenye matukio hayo.
Alex alikuwa akiwakamata watoto hao majira ya usiku na wengine mchana kwa kuwatishia kuwa yeye ni Polisi au Ustawi wa Jamii akidai kuwa anakamata watoto wazururaji kisha kwenda kuwabaka.