Klabu ya soka ya Simba SC, imeondolewa kwenye mashindano ya African Football League kwa kukubali goli moja la ugenini dhidi ya Al Ahly, na kufanya mchezo huo kuisha kwa Agg: 3-3.
Tarehe 20, mwezi huu Simba ilikutana na Al Ahly kwenye dimba la Mkapa kwenye ufunguzi wa ligi hiyo na kufanikiwa kuondoka na goli mbili kwa mbili.