Mwanamke mmoja huko nchini Indonesia mwenye umri wa miaka 70 ameolewa na kijana wa miaka 16.
Baada ya video za ndoa hiyo kusambaa mitandaoni, wanandoa hao wakasema wao wamefanya hivyo kwa siri, kwani sheria za nchi hiyo hairuhusu kijana wa miaka hiyo kuoa na ndio maana hawajasajili ndoa yao kwenye daftari la Serikali.
Sheria ya Indonesia, inaruhusu msichana wa umri kuanzia miaka 16 kuolewa, na kwa mvulana wa umri kuanzia miaka 19 anaruhusiwa kuoa.