Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Rais Samia mgeni rasmi siku ya kupiga vita madawa ya kulevya

Maadhimisho Ya Kitaifa Ya Kupiga Vita Dawa Za Kulevya Yanatarajiwa Kufanyika Kesho Juni 25 Jijini Arusha Na Mgeni Ni rais Wa Jamuhuri Ya Muungano Dkt Samia Suluhu Hasani .

Mratibu Wa Shughuli Hiyo Dkt Said Mkwizu Ambaye Ni Afisa Tiba Inayosaidia Warahibu Dawa Za Kulevya Kutoka Taasisi Isiyo Ya Kiserikali Mat Amesema Watu Wajitokeza Kwa Ajili Ya Kupata Ushauri Wa Kitaalamu Kuhusiana Na Watumiaji Wa Dawa Za Kulevya.

Kwa Upande Wake Dkt Sosteus Ambaye Ni Msimamizi Wa Clinic Ya Warahibu Wa Dawa Za Kulevya Katika Hospitali Ya Mkoa Mwanayamala, Amesema Watumiaji Wengi Wa Dawa Za Kulevya Wanarudi Kutumia Dawa Hizo Kutokana Na Tiba Hiyo Kuchukua Muda Mrefu Kama Magonjwa Mengine.

Juni 26 Ni Siku Ya Siku Ya Kimataifa Ya Kupinga Matumizi Mabaya Ya Dawa Ya Kulevya Na Inaadhimishwa Kila Mwaka Kwa Lengo La Kuifanydunia Kuwa Huru Kwenye Matumizi Ya Dawa Za Kulevya.

Siku Hii Imekuwa Ikiadhimishwa Tangu Kupitishwa Na Baraza Kuu La Umoja Wa Mataifa, Desemba 1987 Kama Sehemu Ya Juhudi Za Ulimwengu Kuchagiza Vitendo Na Ushirikiano Ili Kushinda Vita Dhidi Ya Matumizi Ya Dawa Za Kulevya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *