Serikali Mkoani Shinyanga Imeuagiza Uongozi Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Shinyanga Kuhakikisha Wanaongeza Juhudi Za Ukusanyaji Mapato Ili Waweze Kufikia Malengo Waliyo Jiwekea Ya Kukusanya Mapato Kwa Asilimia 100 Ndani Ya Siku 7.
Maagizo Hayo Yametolewa Na Mkuu Wa Mkoa Wa Shinyanga Christina Mndeme Katika Mkutano Maalum Wa Baraza La Madiwani Walioketi Kwa Ajili Ya Kupokea Kupitia Na Kujadili Hoja Ya Mkaguzi Mkuu Wa Hesabu Za Serikali CAG Kwa Mwaka Wa Fedha 2021/2022.
Aidha Mndeme Amebainisha Kuwa Kuanzia Mwezi Julai 2022 Hadi Juni 19, 2023 Wamefikia Asilimia 74 Ya Ukusanyaji Wa Mapato Na Kueleza Kuwa Kiasi Cha Asilimia 26 Bado Kinahitajika Kukusanywa Ndani Ya Siku 7 Ili Kufikia Malengo Waliyojiwekea Ya Kukusanya Mapato Kwa Asilimia 100.
Akizungumza Kwa Niaba Ya Madiwani Mwenyekiti Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Shinyanga Bw.Ngassa Mboje Ameahidi Kushirikiana Na Wataalamu Katika Halmashauri Hiyo Kutekeleza Maagizo Yote Yaliyo Tolewa Na Mkuu Wa Mkoa .