Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Bilioni 325 zawezesha miradi 9 ya kitaifa kupitia Tanroads mkoani Shinyanga

Wakala wa Barabara Tanzania(TANROADS) Mkoa wa Shinyanga katika kipindi cha miaka mitatu kati ya 2021/2024 inatekeleza miradi mikubwa tisa ya kitaifa ambayo ni pamoja na ujenzi wa uwanja wa ndege wa Ibadakuli, ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Lamadi kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 50.3 pamoja na barabara Kagongwa-Bukooba-Nzega yenye urefu wa Kilomita 66 kati ya hizo 11 zikipatikana mkoani Shinyanga.

Taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari na Kaimu Meneja Wa TANROADS mkoa wa Shinyanga Mhandisi Samwel Joel Mwambungu hivi karibuni imeanisha miradi mingine kuwa ni barabara ya Kahama-Kakola yenye urefu wa kilomita 73 kwa kiwango cha lami pamoja na kufanyika kwa upembuzi yakinifu katika barabara za Kolandoto-Lalago yenye urefu wa kilomita 53, Salawe-Old Shinyanga yenye urefu wa kilomita 64.66, Uyogo-Nyamilagano-Nyandekwa-Kahama ambayo kilomita 54 zipo Shinyanga na upembuzi wake umekamilika.

Aidha katika kipindi hicho Tanroads pia imefanya usanifu katika barabara ya Old Shinyanga- Bubiki yenye urefu wa kilomita 35 pamoja na barabara ya Kahama-Solwa yenye urefu wa kilomita 76.69 ambayo upembuzi wake umekamilika

Wakati huo huo katika kukabiliana   na athari za mvua za Elnino,serikali kupitia Tanroads ilitenga na kutoa fedha za dharura kiasi cha shilingi  bilioni 1.3 zilizonufaisha barabara ya Kahama-Solwa yenye urefu wa kilomita 79.96 na kufanikisha urejeshaji wa mawasiliano ya barabara hiyo iliyokuwa imekatika.

Pia kiasi cha Shilingi bilioni 1.18 zimetumikak katika usimikaji wa taa za mwanga barabarani katika miji na vijiji vya Tinde,Isaka,Kagongwa,Kahama,Segese na Bulige ikiwa ni pamoja na taa zinazotarajiwa kufungwa katika maeneo ya vijiji vya Solwa na Ngaya.

Katika kipindi cha miaka mitatu madarakani ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan mkoa wa Shinyanga umepokea kiasi cha bilioni 325 zilizotumika katika miradi matengenezo ya barabara ili kuziwezesha kupitika katika kipindi chote cha mwaka hatua iliyoboresha miundombinu katika bararabara zenye urefu wa kilomita 1177.74 na madaraja 309 yaliyo chini ya wakala wa barabara Tanzania(TANROADS) mkoa wa Shinyanga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *