Kesi ya Marioo ya madai ya Mil 550 kusikilizwa Machi 18 na 19

Staa wa muziki wa Marioo, anatarajiwa kupanda Mahakama Kuu Masjala ya Wilaya ya Arusha kujitete ifikapo Machi 18 na 19, mwaka huu.



Marioo na Meneja wake Sweetbert Mwinula wameshtakiwa katika Mahakama Kuu Masjala ya Wilaya ya Arusha mbele ya Jaji Joackim Tiganga, wakidaiwa jumla ya Sh. 550,000,000 kwa madai ya kuvunja mkataba wa kutumbuiza katika hafla ya Mr & Miss Vyuo Vikuu Kanda ya Kaskazini.

Mdai katika shauri hilo ni Kampuni ya Kismaty inayojihusisha na kuandaa matukio ya burudani mbalimbali nchini.

Mdai anayewakilishwa na Wakili John Lairumbe, anadai kuwa Septemba 23, 2021, aliingia mkataba na wadaiwa kutumbuiza siku ya mashindano hayo kwa gharama ya Sh. milioni 15.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *