Biashara ya ngono imewachosha, wakimbilia Polisi

Wananchi wa Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza wameiomba Serikali kuwachukulia hatua watu wanaofanya biashara ya ngono katika eneo hilo kwani kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la madanguro.

Akielezea kero hiyo mmoja wa wananchi wa eneo hilo Abdulmajdi Fadhil amesema kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la madanguro katika eneo hilo hali ambayo imekua ikifanya eneo hilo liwe na ongezeko la wakina dada wanaotoka sehemu nyingine kwa lengo la kufanya biashara ya kujiuza.

Aidha wananchi hao wameliomba jeshi la polisi liweze kufanya msako wa madawa ya kulevya kwani kumekuwa na mianya ya uuzaji wa madawa ya kulevya hali ambayo imekuwa ikiharibu vijana wengi wanaotumia madawa hayo.

Akijibu kero hiyo Kamanda wa Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza (SACP) Wilbroad Mutafungwa amesema Jeshi la polisi ndani ya Mkoa huo halipo tayari kuona biashara za madanguro na pamoja na zile za madawa ya kulevya zikiwa zinaendelea hivyo jeshi hilo linakwenda kuanzisha operesheni ili kutokomeza matendo yote ya uovu ndani ya mkoa huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *