Yanga yataka kuweka rekodi ligi ya mabingwa

Meneja Habari wa Yanga SC, Ally Kamwe amesema malengo yao msimu huu kwenye mashindano ya ligi ya mabingwa afrika, ni kufika hatua ya Makundi, maana hawajawahi kufanya vizuri kwenye mashindano hiyo.

“Malengo yetu msimu huu Kimataifa ni kuhakikisha tunatinga hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani AFRIKA, mashindano ambayo hatujashiriki kwa muda mrefu, tumeshafanya vizuri kwenye mashindano ya shirikisho na sasa malengo yetu ni kufanya vizuri kwenye ligi ya mabingwa” amesema Kamwe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *