Malasusu Askofu mpya KKKT

Mkutano Mkuu wa 21 wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) umemchagua Askofu Alex Malasusa kuwa mkuu mteule wa KKKT.

Askofu Malasusa wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani anachukua nafasi ya Askofu Fredrick Shoo aliyemaliza muda wake wa uongozo wa awamu mbili.

Anarejea tena kwenye nafasi hiyo aliyoihudumu kuanzia 2007-2015 alipomaliza na nafasi yake ikiongozwa na Askofu Shoo.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo mwenyekiti wa uchaguzi huo,Askofu Amon Mwenda,amesema kura zilizopigwa zilikuwa 241 ambapo kati ya hizo Malasusa amepata kura 167 sawa na asilimia 69.3 huku Askofu Abednego Kesho Mshahara akipata kura 73 sawa na asilimia 30.3

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *