Pamba jiji yashusha Nyanda wa Dodoma jiji

KLABU ya Pamba Jiji FC imetangaza kumsajili aliyekuwa golikipa wa Dodoma jiji FC msimu uliopita, Rahem Shekh kuwatumikia wakali hao wa Jiji la miamba kwenye msimu wa 2023/24 wa ligi ya Championship Tanzania bara.

Raheem anarejea kwa mara ya pili jijini Mwanza baada ya kuitumikia Mbao FC katika msimu wake wa mwisho wa kucheza ligi kuu bara, ambapo baada ya Mbao FC kushuka alijiunga na KMC kisha Dodoma Jiji FC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *