Na Eunice Kanumba
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha amekabidhi gari jipya lenye nambari za usajili STN 2943 Toyata Hilux pick up double cabin kwa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini katika mkoa huo lililotolewa na serikali kupitia wizara ya maji lengo likiwa kuongeza ufatiliaji na usimamzi katika miradi ya maji inayoendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Hafla hiyo ya makabidhiano ya gari imefanyika leo tarehe 28 Oktoba, 2024 katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, pamoja na watumishi mbalimbali kutoka RUWASA na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
“Kwanza tumshukuru na kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwawezesha watumishi katika Wizara, Sekta na Ofisi zake zote ili kurahisisha utekelezaji na usimamizi wa shughuli za kila siku kama ambavyo imefanyika kwa wenzetu hawa RUWASA”amesema RC Macha.
Aidha RC Macha ameitaka RUWASA kuhakikisha kuwa gari hilo linatunzwa kwa maslahi mapana ya Serikali ili lidumu muda mrefu na lifanyiwe matengenezo stahiki pale inapohitajika kufanya hivyo ili gari hilo litumike kwa vizazi na vizazi.
Kwa upande wake Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Julieth Payovela ameishukuru serikali kuwapatia gari hilo kwani litakwenda kuongeza ufanisi katika ufatiliaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa katika mkoa wa Shinyanga huku amkimshuru mkuu huyo wa mkoa kwa kuendelea kutoa ushirikano kwa wakala hiyo katika kutimiza majukumu mbali mbali.
One response to “Rc Macha Akabidhi Gari Jipya Kwa Ruwasa Mkoa Wa Shinyanga.”
Hongera jambo Media👏👏👏