Wazazi na jamii kwa ujumla wametakiwa kuwalea watoto katika malezi ya maadili mema bila kujali aina ya uhusiano uliopo baina yao na kuepuka kuwabagua kwa namna yeyote.
Nasaha hizo zimetolewa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Habib Makusanya kupitia mahojiano maalum aliyofanya na Jambo FM akiwa ofisini kwake na kuelezea kusikitishwa kwake na uwepo wa mmomonyoko wa maadili miongoni mwa vijana ndani ya jamii.
Aidha ameeleza kwamba ili kufanikisha azma ya malezi bora ndani ya familia wazazi wanapaswa kuwa kielelezo cha upendo miongoni mwao hatua itakayowawezesha watoto kuiga mifano bora kuanzia ndani ya ngazi ya familia pamoja na wanaume kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ndani ya familia.
Akielezea hofu yake juu ya mienendo ya Vijana na matokeo yake katika Taifa amesema iwapo vijana wakikosa malezi yaliyojengwa katika misingi ya imani ya dini zao Sheik Makusanya amebainisha kuwa kwa hapo baaadaye taifa linaweza kukosa viongozi wenye maadili kutokana kutokuwa na hofu ya Mungu.