Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Meseji za Mume na Mchepuko zapelekea Mke kujiua

Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa Jina la Marietha Bosco Sagana (32) mkazi wa kitongoji cha Matarawe, kijiji cha Marungu kata ya Tingi ,tarafa ya mpepo Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma amefariki Dunia baada ya kunywa sumu chanzo kikiwa ni wivu wa Mapenzi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma ACP-Marco Chilya, amesema tukio hilo limetokea Novemba 8,2023 Majira ya Saa mbili za Usiku, ambapo siku ya tukio Mume wake alikuwa amekwenda Shambani lakini alisahau simu yake Nyumbani ndipo Marietha alivyoiona simu hiyo akaanza kuipekua na kusoma Meseji na kukuta Meseji nyingi za Mume wake na Mwanamke Mwingine.

Marehemu baada ya kusoma Meseji hizo alishindwa kuvumilia ndipo akachukua Dawa ya kuulia Wadudu kwenye mahindi (Actellic ) akaikoroga na kuinywa na baadaye aliishiwa nguvu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *