Jambo La Leo

Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mke wa Askofu ajinyonga

Mke wa Askofu Vitalis Yusuph Askofu wa Kanisa la Angilikana Dayosisi ya Biharamulo aliyetambulika kwa jina la Monica Zabron Mkazi wa kijiji cha Kasenga kata ya Kasenga Wilaya ya Chato Mkoani Geita amekutwa amefariki dunia kwa kujinyonga karibu na kambi ya Hifadhi ya Burigi iliyopo wilayani Chato mkoani Geita.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Geita Kamishina Msaidizi wa Polisi Safia Jongo amesema tukio hilo limetokea Novemba 8 2023 majira ya saa tisa mchana katika kijiji hicho ambapo amesema sababu za Mwanamke huyo kujinyonga ni kuugua saratani kwa muda mrefu.

Kamanda Jongo ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi kuacha kuchukua hatua ya kujitoa uhai kwa sababu yoyote ikiwemo ugojwa na kuongeza kuwa ni vyema wakafika katika hospitali mbalimbali kwa ajili ya ushauri wa madaktari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *