UVCCM waipa Serikali siku 7 kutoa majibu Mikopo ya 10%

Baraza Kuu la Umoja wa Vijana CCM ( UVCCM ) Taifa limeitaka Serikali kutoa majibu kwa Vijana ni lini mikopo ya 10% itarejeshwa baada ya kusitishwa kwa miezi kadhaa na kwamba limeipa Serikali siku 7 kutoa majibu na isipofanya hivyo basi Wizara husika zijitathmini kama zinatosha kusimamia maslahi ya Vijana.

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mohammed Kawaida amesema hayo Mkoani Kigoma baada ya Baraza hilo kumaliza vikao vyake vilivyofanyika Mkoani humo na kutoka na maazimio hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *