Karamoko aliyeitosa Yanga, ajiunga na ‘Bundesliga’

Mshambuliaji wa klabu ya Asec Mimosas, Karamoko Sankara amejiunga na klabu ya Wolfsberger AC inayoshiriki Ligi Kuu Austria ‘Bundesliga’.

Asec Mimosas kupitia mitandao ya kijamii imebainisha kuwa kinara huyo wa mabao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, amesaini mkataba wa miaka mitatu na miamba hiyo ya Austria ambayo inakamata nafasi ya saba kwenye msimamo wa ‘Bundesliga’

Sankara anaungana na mshambuliaji wa zamani wa Asec Mimosas, Karim Konate ambaye pia anachezea Bundesliga kunako klabu ya RB Salzburg.

Taarifa ya klabu ya Wolfsberger AC imesema:- “Mshambuliaji mpya wa Wolves. RZ Pellets WAC inatangaza kumsajili mshambuliaji chipukizi Sankara Karamoko.”

Yanga SC ya Tanzania, ni miongoni mwa timu zilizokuwa zikiifukuzia saini yake, ili Kuongeza nguvu eneo la ushambuliaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *