Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Afisa Elimu kizimbani kwa kusababisha vifo vya watu watatu

Afisa Elimu Taaluma wilayani Kwimba mkoani Mwanza, Samwel Kulinga (44) amefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka manne likiwemo la kuendesha gari kwa mwendokasi, kuwagonga na kuwasababishia vifo watu watatu.

Katika kesi hiyo namba 5383/2024 kulinga amesomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kwimba, Dastan Ndeko. Akisoma mashtaka hayo Wakili wa Serikali Frank Nchanila amesema shtaka linguine linalomkabili afisa elimu huyo ni kuendesha gari bila ya leseni katika barabara ya Umma.

Hata hivyo, mshtakiwa ameachiwa huru baada ya kukidhi masharti ya dhamana ambayo ni kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua ya utambulisho kutoka kwa kiongozi wa wa Serikali za mitaa, mdhamini atakayesaini bondi ya mali isiyohamishika yenye thamani ya TSh 5 milioni na nakala ya Kitambulisho cha Taifa (Nida) ama Mpiga Kura.

Hakimu huyo, ameahirisha shauri hilo hadi Februari 19, 2024, litakapoitwa kwa ajili ya mshtakiwa kuanza kusomewa hoja za awali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *