Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto Grayson Kanyenye wamefikishwa tena Mahakamani leo Januari 13, ikiwa ni mara ya pili kupandishwa kizimbani wakikabiliwa na shtaka la kumuua kwa makusudi mtoto huyo siku ya Desemba 25, 2024
Washtakiwa hao wawili ambao ni Tumaini Msangi na Kelvin Gilbert wote wakazi wa Ipagala Jijini Dodoma wamefikishwa Mahakamani hapo leo mbele Hakimu mkazi daraja la kwanza Charles Eligi.
Awali, Wakili upande wa Jamhuri Wakili wa Serikali Mwandamizi Patricia Mkina aliiomba Mahakama kupanga tarehe nyingine kwaajili ya kutajwa ndipo Hakimu Eligi akaahirisha shauri hilo namba 3000551 la mwaka 2024 hadi Januari 27, 2025 litakapotajwa tena kutokana na Hakimu anayesimamia Kesi hiyo Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Denis Mpelembwa kuwa na udhuru .
Washtakiwa watarudi Mahabusu kutokana na shauri lao kutokudhaminika.
Ikumbukwe kuwa watuhumiwa hao walifikishwa Mahakamani hapo kwa mara ya kwanza siku ya tarehe 30 Desemba, 2024 ambapo hawakutakiwa kujibu chochote


