Upasuaji mdogo wa moyo wa kubadilisha valvu ya mshipa mkubwa wa damu (Aortic Valve) bila kufungua kifua (Transcatheter Aortic Valve Implantation procedure – TAVI),umefanyika kwa wagonjwa watatu wenye umri wa zaidi ya miaka 70 katika kambi maalumu ya matibabu ya siku mbili iliyofanywa na wataalamu wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu wa JKCI na wenzao wa Hospitali ya Starcare ya nchini India.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. John Jingu amesema uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika sekta ya afya hii ikiwa ni pamoja na kujenga majengo ya kisasa, kusomesha wataalamu na kuunua vifaa tiba vya kisasa kumewezesha kufanyika kwa upasuaji huo.
Dkt. Jingu amesema kutokana na umuhimu mkubwa wa sekta ya afya Serikali itaendelea kuboresha huduma ya afya ikiwa ni pamoja na kusomesha wataalamu katika nchi mbalimbali ambao watakuja kutoa matibabu ya kibingwa nchini.
Kwa Julai hadi Disemba mwaka huu alidokeza kuwa JKCI imehudumia zaidi ya wagonjwa 3,000 katika kufanya upasuaji mkubwa na mdogo wa moyo na kusisitiza Serikali itaendelea kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kibingwa za