RC KIHONGOSI AKEMEA TABIA YA TANROADS KUTOA TENDA KWA KUJUANA..

Mkuu wa mkoa wa Simiyu Kenani Kihongosi amwataka mamlaka ya barabara Tanroads mkoani humo kuacha kuwapa makandarasi wasio na sifa na kwa kujuana kutekeleza miradi ya barabara licha ya kutokidhi vigezo na badala yake wamekua wakifanya kazi zilizo chini ya viwango na kutia hasara nchi kwa kutumia bure kodi za wananchi.

Kihongosi ametoa maelekezo hayo wakati wa kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Bariadi Conference kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa miradi ya barabara huku akikemea kuharibika kwa miundombinu hiyo mara kwa mara hali inavyogharimu serikali marekebisho ambayo yangeweza kuepukika.

“Unampa mkandarasi kwa kuwa mnajuana mlisoma pamoja hana vigezo wala vifaa mwisho wa siku barabara haina miezi sita inahitaji marekebisho imejaa mashimo haya mashimo yatakuja kuleta madhara makubwa” kihongosi

Akitolea ufafanuzi barabara ya Lamadi – Mwanza ambayo hivi karibuni imesababisha ajali ya basi la kisire linalofanya safari zake Musoma Mwanza baada ya kukwepa shimo, mwakilishi wa Tanroads Mhandisi Mohammed Athuman amesema kuwa barabara hiyo ni kongwe na inahitaji kujengwa upya. 

“Barabara hiyo ina zaidi ya miaka arobaini kweli ni chakavu na hata marekebisho hayatokidhi barabara yote kwa kuwa inahitaji kujengwa upya tunaitegemea serikali kuweza kutupatia pesa kwa ajili ya ujenzi huu ili tuondokane na hizo ajali” Mhandisi Athuman.

Mbunge wa jimbo la itilima Njalu Silanga amesema kuwa barabara ya Itilima kwenda Meatu ambayo ni kiungo muhimu na ile ya Ligangabilili kwenda Singida ambayo kwa sasa ipo na hali korofi ilikuwa imesanifiwa kujengwa kwa kiwango cha lami lakini ilicheleweshwa kutokana na kuchelewa kwa mvua lakini tayari wakandarasi wameshapeleka mitambo kwa ajili ya kuanza ujenzi.

“Walijua mvua zitawahi ndo maana wakachelewa kupeleka mitambo lakini kwa sasa tayari waesha peleka ndani ya siku chache zijazo kazi itaanza ili wananchi wasiendelee kupata adha ya mawasiliano ya barabara na maeneo korofi zaidi tunayafanyia marekebisho ya haraka ili waendelee kupata huduma” Njalu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *