MILIONI 90 ZATOLEWA NA MANISPAA SHINYANGA KWENDA KWENYE VIKUNDI HIVI….

NA  EUNICE KANUMBA-SHINYANGA  

Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Desemba 20,2024 imekabidhi Mikopo ya asilimia 10 yenye thamani ya shilingi Milioni 90,000,000 itokanayo na mapato ya ndani ya Halmashauri kwenye vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Akikabidhi hundi ya mikopo hiyo Mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko amevitaka vikundi hivyo kuwa na nidhamu ya pesa pamoja na matumizi sahihi kulingana na andiko la miradi yao waliwasilisha katika halmashuri hiyo.

“Serikali inatoa mikopo hii kwa lengo la kupunguza wimbi kubwa la vijana wasio na ajira, kuweni na nidhamu na fedha hizi, kama ambavyo maandiko yenu ya miradi yameonyesha ndivyo hivyo fedha hizi zikatumike.Fedha hizi zisiwe chanzo cha matatizio na migogoro” Amesema  Elias Masumbuko 

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Dkt. Elisha Robert amesema manispaa hiyo itaendelea kutoa fedha kwa vikundi vyote vitakavyokidhi taratibu zote kama taratibu  za  serikali zinavyoelekeza. 

“Lengo la serikali ni kuhakikisha kila mwananchi ananufaika na mikopo hii, Halmashauri itaendelea kutoa mikopo hii kadri ya vikundi vitakavyo kidhi taratibu, nitumie fursa hii tu kuwaasa wananchi wenye sifa kuunda vikundi ili wewezekupata mikopo hii ili kupambana na ukosefu wa ajira na kuondokana na umaskini” Amesema Dr Elisha.

Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya jamii halmashauuri ya manispaa ya Shinyanga Salome Komba ameainisha kuwa jumla ya vikundi vitatu vimepatiwa  mikopo hiyo  ambapo kikundi cha VIJANA SEAT COVER cha vijana kutoka kata ya Kambarage ambacho kimepatiwa mkopo wa Shilingi 50,000,000, kwa ajili ya kutengeneza  seat cover za magari  pamoja na kikundi cha FIVE MAMA’s cha wanawake kutoka kata ya Ngokolo, ambacho kimepatiwa shilingi milioni 20,000,000 kwa ajili ya kufanya biashara ya duka la nguo na utengenezaji wa mikoba pamoja uuzaji wa viatu vya mitumba.

Ili kuthamini watu wenye ulemavu manispaa hiyo imempatia mkopo mlemavu wa ngozi anayeishi kata ya ndala manispaa ya Shinyanga Higini Mwacha ambaye amepatiwa mkopo wa shilingi milioni 20,000,000 ili kufanya biashara ya vifaa vya ujenzi 

 pamoja na Mtu mwenye ulemavu kutoka kata ya Ndala kiasi cha shilingi 20,000,000 kwa ajili ya duka la vifaa vya ujenzi, ambapo mikopo hiiyo imetolewa chini ya Sura ya 290 na kanuni zake  chini ya kifungu cha 37A (4) zinazojulikana kama kanunu za utoaji na usimamizi wa mikopo kwa vikundi vya Wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *