JAMBO YAZINDUA SELEBRETIKA KIJAMUKAYA, WITO MAALUM WATOLEWA KWA WATUMIAJI……

NA EUNICE KANUMBA ,SHINYANGA

Kampuni ya jambo group, imezindua kampeni ya Selebretika Kijamukaya kwa kuzalisha vinywaji vikiwa na chapa au Logo maalumu kwa ajili ya msimu huu wa sikukuu za Christmas na Mwaka mpya.

Uzinduzi wa kampeni hiyo umefanyika leo Jumamosi Desemba 21,2024 kwenye Makao makuu ya Ofisi za Jambo zilizopo Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.

Kiongozi Mkuu wa Jambo Media, Nickson George ambaye pia ni kiongozi wa ubunifu na msimamizi wa chapa Jambo Group, amesema kampeni hiyo ya selebretika kijamukaya ni kwa ajili ya wateja wao na watumiaji wote wa bidhaa za kampuni hiyo kufurahia bidhaa za jambo wakiwa na familia zao katika msimu mzima wa sikukuu.

“Leo ni siku muhimu kwetu sisi makampuni ya Jambo Group, kwa sababu tunazindua kampeni yetu ya msimu wa sikukuu iitwayo Selebretika Kijamukaya ambapo tumezalisha vinywaji maalumu vikiwa na chapa au nembo kwa ajili ya msimu wa sikukuu na hii tumefanya ili kuleta ladha nzuri ya kusheherekea kinyumbani zaidi’. amesema Nickson George.

“Ili nyumbani paweze kunoga na sikukuu iweze kuwa tamu zaidi unapo selebretika kijamukaya hakikisha nyumbani kwako kuanzia asubuhi mpaka jioni kuna kuwa na bidhaa za jambo, asubuhi ukiamka kuna vitafunwa vya jambo, maji ya jambo, juice za jambo, biskuti za jambo, Ice crem za jambo na ukikosa vinywaji ya jambo kwenye meza yako sikukuu haiwezi kunoga,”ameongeza.

Pia, Nickson ametoa wito kwa wananchi wa kanda ya ziwa au mikoa yote ambayo bidhaa za jambo zinapatikana na kwamba kama wameshidwa kufika nyumbani kufurahi na familia, watume hata katoni mbili za juice ya jambo dodo, soda, maji na mikate ya jambo na ambao wanasafiri watumie bidhaa za jambo, ili waselebretike kijamukaya katika msimu huu wa sikukuu.

Nickson ameongeza kwa kusema lengo la kampeni hiyo ni kuona watu wote wanasheherekea sikukuu wakiwa na familia zao na wale ambao watashindwa kujumuika kutokana na majukumu, basi wawapigie simu na kuwatakia heri ya Kristimas na mwaka mpya, pamoja na kutuma kitu chochote ili wafurahie, sababu familia ni sehemu ya kwanza ambayo inatengeneza msingi wa amani yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *