Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Samia: Viongozi wa kisiasa wanaongoza kwa rushwa

Rais Samia Suluhu Hassan Amesema Moja Ya Vikwazo Vya Maendeleo Barani Afrika Ni Pamoja Na Janga La Rushwa Ambalo Limekuwa Likidhoofisha Mifumo Ya Kitaasisi Na Kuathiri Mipango Na Mikakati Ya Kujikomboa Kiuchumi.

Kauli Hiyo Ameitoa Leo Aliposhiriki Maadhimisho Ya Siku Ya Kupambana Na Rushwa Afrika Yaliyofanyika Mkoani Arusha, Ambapo Amesema Vitendo Hivyo Haviishii Kwenye Mipaka Ya Nchi Kwa Kuwa Ni Miongoni Mwa Makosa Yanayovuka Mipaka.

Aidha Rais Dkt. Samia Amewataka Wadau Wa Mapambano Ya Rushwa Kupambanua Na Kubainisha Vikwazo Dhidi Ya Vita Hiyo Na Kuchukua Hatua Muafaka,Na Kuongeza Kuwa Dunia Itambue Kuwa Afrika Si Salama Kwa Wala Rushwa Na Si Kichaka Cha Ufichaji Wa Fedha Zinazotokana Rushwa Hiyo.

Katika Hatua Nyingine Rais Ametaja Maeneo Mbalimbali Ambayo Yameonekeana Kuwa Yanaongoza Kwa Rushwa Hapa Nchini Ambapo Katika Hatua Ya Kwanza Rais Samia Amesema Kwamba Viongozi Wa Kisiasa Ni Miongoni Mwa Watu Ambao Wanaongoza Kwa Rushwa Hapa Nchini.

Sehemu Nyingine Zilizotajwa Na Raisa Ni Polisi, Mahakamani, Vyuoni Na Maofisini, Ambapo Maeneo Hayo Yaliyotajwa Ni Kwa Mujibu Wa Takwimu Pamoja Na Ushahidi Wa Picha Ambao Umetolewa Katika Kuthibitisha Jinsi Ambavyo Rushwa Inaonekana Kushamiri Kwa Kasi Katika Maeneo Hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *