Rais wa Romania Klaus Iohannis, amesema nchi hiyo itashirikiana na Tanzania kuhakikisha ajenda zake kwenye medani za kimataifa zinafanikiwa ikiwa ni pamoja na ajenda ya nishati safi ambayo itapelekwa kwenye mkutano wa Mazingira Duniani unaotarajiwa kufanyika katika Falme za Kiarabu.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina yake na Rais Samia, Rais Iohannis amesema nchi hiyo ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali kimataifa.
Rais huyo pia anatarajiwa kwenda Zanzibar ambapo atakutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi ili kujifunza zaidi kuhusiana na utekelezaji wa sera ya uchumi wa Buluu.