RAIS SAMIA ATUA DODOMA NA TUZO YA KIMATAIFA “THE GLOBAL GOALKEEPER AWARD”

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili Uwanja wa Ndege Mkoani Dodoma akiwa amebeba Tuzo Maalum ya Kimataifa ya “The Global Goalkeeper Award” aliyokabidhiwa leo February 04, 2025 na Rais wa Kitengo cha Usawa wa Jinsia kutoka Taasisi ya Gates, Dkt. Anita Zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili uwanjani hapo, Rais Samia amesema tuzo hiyo ni zawadi kwa Watoa huduma wote wa Sekta ya Afya ambapo amewapongeza kwa kazi kubwa wanayofanya katika kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto.

Rais Samia ndiye Rais wa Kwanza Barani Afrika kupata tuzo hiyo ya Kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *