Wananchi wa Mkoa wa Geita wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kumaliza mgogoro wa vigingi baina ya Mgodi wa Uchimbaji madini ya dhahabu Geita (GGM) na wananchi wanaozunguka mgodi uliodumu kwa kipindi cha miaka 23 kuanzia mwaka 1999 hadi 2023.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Novemba 11 kwenye kituo cha afya Kabuku wilayani Handeni, ambapo Mama wa Marehemu Khadija Athuman amesema walipofika katika kituo cha Afya kabuku walinyanyaswa na watoa huduma hali iyopelekea mwanae kushindwa kufanyiwa Oparesheni.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Handeni Albert Msando amekiri kutokea kwa Kifo cha Mjamzito huyo ambapo amesema baada ya kufuatilia Mama huyo alipewa huduma ya Drip peke yake na ilipofika Majira ya Alfajiri alipoteza Maisha.