Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mjamzito afariki baada ya kukosa 150,000 ya oparesheni

Mama mjamzito aliefahamika kwa jina la Mariam Zahoro mwenye umri wa miaka 39 aliyekuwa akiishi kwenye kijiji cha Mumbwi wilayani Handeni mkoani Tanga amefariki dunia akiwa kwenye kituo cha afya Kabuku kilichopo wilayani humo ikidaiwa kuwa alikosa huduma ya upasuaji baada ya kushindwa kulipa kiasi cha shilingi Laki moja na elfu hamsini alizotakiwa kutoa kwa ajili ya huduma hiyo.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Novemba 11 kwenye kituo cha afya Kabuku wilayani Handeni, ambapo Mama wa Marehemu Khadija Athuman amesema walipofika katika kituo cha Afya kabuku walinyanyaswa na watoa huduma hali iyopelekea mwanae kushindwa kufanyiwa Oparesheni.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Handeni Albert Msando amekiri kutokea kwa Kifo cha Mjamzito huyo ambapo amesema baada ya kufuatilia Mama huyo alipewa huduma ya Drip peke yake na ilipofika Majira ya Alfajiri alipoteza Maisha.

11:36 AM

Jack JAMBO FMadmin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *