Michuano ya AFCON 2023 Kundi F leo saa 5:00 usiku litamaliza mechi za hatua ya makundi kwa Tanzania kuivaa DR Congo huku Morocco ikiikabili Zambia.
Katika kundi hilo Morocco anaongoza kwa pointi 4, DR Congo 2, Zambia 2 na Tanzania 1, hivyo ushindi kwa Tanzania utaiweka sehemu nzuri ya kufuzu hatua ya 16 bora.