Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Baba amkata kichwa mtoto wake na kumuweka kwenye ndoo

Amedius Mfoi ( 25) Mkazi wa Muriet Jijini Arusha, dereva bodaboda ,anashikiliwa na Jeshi la polisi kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wake wa miaka 3, Amani Amedius Mfoi ,kwa kumkata shingo na kitu chenye ncha kali na kutenganisha kichwa na kiwiliwili, ambapo babu na bibi wa Aman, wamesema walimuacha mjukuu wao nyumbani akiwa na baba yake na waliporudi walikuta mjukuu wao amekatwa kichwa na kuwekwa kwenye ndoo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo ,amesema kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Januari 23,2024 na kuongeza kuwa , baada ya uchunguzi Jalada litapelekwa ofisi ya taifa ya mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *