Huduma bora kwa wananchi lazima tija na maslahi viwe na uwiano -Ndejembi

Naibu Waziri ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia elimu Deogratius Ndejembi amesema ili kuwepo na matokeo bora ya kiutendaji kazi katika kutoa huduma bora kwa wananchi lazima tija na maslahi viwe na uwiano.


Ndejembi ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha baraza la wafanyakazi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI cha kupitisha bajeti na mpango kazi kwa mwaka 2024/25.


Aidha amewasisitiza kuwa mikutano ya mabaraza ya wafanyakazi itumike katika kujadili malengo na mipango ya taasisi ikiwa ni pamoja na maslahi ya watumishi na kuongeza kuwa mabaraza hayo yanatakiwa kujadili utendaji kazi wa kila siku na jinsi ya kuboresha utendaji kazi zaidi.


Amesema kuwa madhumuni ya baraza la wafanyakazi ni kutoa fursa kwa watumishi kupitia kwa wawakilishi wao kujadiliana juu ya masuala mbalimbali ya msingi yanayohusu tija na ufanisi kwa upande mmoja na maslahi yao kama watumishi kwa upande mwingine.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi na Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Dkt. Charles Msonde amesema baraza la wafanyakazi liliundwa kwa mujibu wa sheria kama yanavyoundwa mabaraza mengine katika uwajibikaji na ndiyo linalounganisha kati ya wafanyakazi na wakuu wa idara wengine na kuwafanya kutimiza wajibu wao katika utendaji wa kazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *