Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Filamu ya kwanza kuigiza Rita Dominic alilipwa 16k

Hii ni stori ya Chanuo kutoka kiwanda cha filamu nchini Nigeria, Rita Dominic ambaye amefanya filamu nyingi sana za kusisimua. Ila mkalio huyu aliigiza filamu ya kwanza na alilipwa N10,000 sawa na Tsh/= 16026.50.

Rita amefunguka hayo katika mahojiano aliyofanya na Joy 99.7 FM kutoka nchini Ghana.

“Nilikuwa na ndoto ya kuwa muigizaji kwa kweli, na wakati huyo Nollywood kulikuwa hakuna pesa. Tulifanya tu kwa sababu tulipenda kazi zetu na tulifanya kwa moyo wetu, kiukweli filamu ya kwanza kufanya niliahidiwa N35,000. Ila nikapwewa N10,000 nyingine Muongozaji akasema atanilipa  mwisho wa mwezi ambayo ilikuwa ni N25,000, lakini hakuwahi kunilipa,” alisema mrembo huyo huku akiwa nacheka.

Kwa sasa muigizaji huyo ni balozi wa makampuni mbalimbali na pia  co-founder wa Audrey Silva Company na CEO wa Rita Dominic Productions. NaDesemba 2023 alityajwa kuwa na utajiri unaofikia kiasi cha Dola Milioni 6.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *