Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Ewura Yawanoa Waandishi wa Habari Shinyanga

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi inayohudumia mikoa ya Shinyanga, Tabora, Katavi na Kigoma imetoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Shinyanga juu ya shughuli za udhibiti wa huduma za nishati na maji kwa lengo la kuimarisha uelewa.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika leo Alhamisi Mei 2,2024 Mjini Shinyanga, Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Mhandisi Walter Christopher amesema waandishi wa habari ni kundi muhimu na kwamba wakielimishwa vizuri na kuwa na uelewa wa kutosha wataandika habari zao kwa usahihi na kuhabarisha umma na kubinisha kwamba kuelimisha Mwandishi wa habari ni kuelimisha jamii.

Akiwasilisha Mada kuhusiana na majukumu ya EWURA,Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mamlaka hiyo Bi.Tobietha Makafu amesema miongoni mwa majukumu ya mamlaka hiyo ni pamoja na kumsimamia mtoa Huduma za nishati na maji ili kuhakikisha anakwenda sambamba na masharti,kanuni,taratibu na sheria za utoaji huduma.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga (SPC) Bw. Patrick Mabula, ameishukuru EWURA kwa semina hiyo na kuahidi kuwa elimu iliyopatikana itatumika kuelimisha wananchi kupitia vyombo vyao vya habari.

Miongoni mwa mada zilizowasilishwa ni pamoja na majukumu na kazi za EWURA na Majukumu ya Ofisi ya Kanda ya Magharibi ya EWURA, ushirikishwaji wa wazawa katika miradi ya petroli na gesi na utaratibu wa kuwasilisha malalamiko EWURA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *