Zaidi ya Bilioni 10 Zitanufaisha Makundi Haya 2024-2025

Na Gideon Gregory,Dodoma

Katika kuelekea mwaka wa fedha 2024/25 Serikali imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 10.5 kwa ajili ya kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa Makundi Maalum hususani wafanyabiashara ndogondogo wakiwemo machinga, mama na baba lishe, waendesha bodaboda na bajaji na makundi mengine yenye biashara ndogo halali zilizosajiliwa, ili  kuyawezesha kugangamala kwa kuyaongeza mitaji na kuboresha shughuli zao za kiuchumi.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt.  Dorothy Gwajima ameeleza hayo leo Mei 17,2024 Bungeni Jijini Dodoma na wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2024/25.

“Katika kutekeleza vipaumbele vilivyoainishwa, Wizara kwa mwaka 2024/25 imekadiria kutumia kiasi cha Shilingi 67,905,259,000, kati ya fedha hizo, Shilingi 47,487,079,000 ni fedha za matumizi ya kawaida ambapo Shilingi 21,650,426,000 ni Fedha za Mishahara na Shillingi 25,836,653,000 ni fedha za uendeshaji wa ofisi, aidha, Shilingi 20,418,180,000 ni fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo kati ya fedha hizo Shillingi 18,025,673,000 ni fedha za ndani na Shillingi 2,392.507,000 ni fedha za nje”amesema Waziri Gwajima.

Ili kufanikisha yote hayo, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imeliomba Bunge kwa mwaka wa fedha 2024/25 liidhinishe jumla Shilingi Bilioni 67.9 ili kutekeleza majukumu yake kwa maendeleo na ustawi wa jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *