Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Anthony Edwards Aipeleka Minnesota Timberwolves Game ya 7

Wakali kutoka Minneapolis Minnesota, Minnesota Timberwolves wakiwa nyumbani Target Center, wamemchapa bingwa mtetezi Denver Nuggets kwa jumla ya vikapu 115-70 na kufanya nusu fainali hiyo ya ligi ya NBA kanda ya Magharibi kwenda ‘Game’ ya 7.

Mnyama mkali Anthony Edwards ndiye alikuwa mkombozi wa Timberwolves, baada ya kupiga pointi 27, Jaden McDaniels akawamaliza kwa kupiga pointi 21 nae Mike Conley akatupia pointi 13 akiwa amerejea uwanjani baada ya kuwa majeruhi.

Kihistoria hakuna bingwa mtetezi wa NBA aliyewahi kupoteza kwenye michezo ya ‘Playoffs’ kwa zaidi ya pointi 36, Denver Nuggets inakuwa timu ya kwanza iliyopoteza kwa tofauti ya pointi 45.

Kesho alfajiri kutakuwa na nusu fainali nyingine ya ‘Game’ ya 6 kanda ya mashariki kati ya Indiana Pacers dhidi ya New York Knicks, iwapo Knicks itashinda itafuzu fainali ya mashariki kucheza na Boston Celtics, kwani Knicks inaongoza kwa ‘Series’ 3-2 na ikiwa tofauti itaenda ‘Game’ ya 7.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *