Picha: Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameweka jiwe la msingi, kuashiria kuzindua rasmi kuanza kwa ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya CCM, katika hafla iliyofanyika eneo la Tambuka reli, jijini Dodoma, litakapojengwa jengo hilo.
Uzinduzi huo uliohudhuriwa na maelfu ya Wananchi wakiongozwa na viongozi na wanachama wa CCM, umefanyika hii leo Mei 28, 2025.





