Zaidi ya Makatibu Meneja 80 wa Vyama vya Msingi vya Ushirika Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, wamepatiwa mafunzo ya ulipaji kodi kwa njia ya mtandao Pamoja utunzaji wa kumbukumbu katika vyama vyao.
Mafunzo hayo, yametolewa na Shirika la Ukaguzi la Vyama vya Ushirika Mkoani Shinyanga (COWASCO), huku Mkaguzi kutoka shirika hilo, Charles Matwiga akisema lengo la la mafunzo hayo pia ni kuwajengea uwezo Viongozi wa Vyama vya Msingi.

Amesema, “Mafunzo hay ani kuwajengea uwezo viongozi wa vyama vya msingi waweze kulipa kodi na kukusanya mapato kitaalamu,lakini zaidi ni kuwawezesha mbinu za kisasa za teknolojia katika kuhifadhi kumbumbuku za vyama vyao.”
Matwiga amesema, katika mafunzo hayo wanavisaidia vyama vyote vya Wakulima kupata TIN namba na kuwajengea uwezo wa namna ya kutumia mfumo wa kulipa kodi.

“Sambamba na hayo tutawasidia kupata TIN namba za vyama vyao lakini zaidi kutumia mfumo wa Malaka ya mapato nchini TRA Kulipa kodi,” ameongezea Matwiga.
Kwa upande wao baadhi ya Makatibu Meneja wa Vyama vya Msingi waliohudhuria mafunzo hayo, wamesema yatasaidia kusimamia mapato ya Serikali na kuongoza vyama vyao kwa misingi thabiti.

“Mafunzo haya yatasaidia katika kukusanya mapato yaserikali kwani hapo awali tulikuwa hatuna elimu na jinsi gani tutaweza kutumia mfumo huu wa TRA lakini itasaidia kusimamia vyama vyetu katika misingi ya Ushirika,” walisema.
COASCO ni shirika la ukaguzi na usimamizi wa vyama vya msingi ambalo jukumu lake kutoa huduma za ukaguzi kwa Vikundi vya Ushirika wa awali, Vyama vya Ushirika, Makampuni binafsi na Umma pamoja na kufanya utafiti na huduma za ushauri.

Kazi yao kubwa ni kukagua hesabu za Vyama vya Msingi vya Ushirika na kutoa elimu ya usimamizi bora wa Fedha na mali za Ushirika katika vyama vya msingi nchini.