Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema WanaCCM wanajukumu la kuibeba Ilani iliyozinduliwa kwa kuendelea kuitangaza, kushawishi watu kuitekeleza.
Ameyasema hayo leo Mei 30, 2025 katika Mkutano Mkuu maalum wa CCM Taifa uliofanyika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya kikwete Jijini Dodoma.

“Nimemtaka katibu Mkuu na Mwenyekiti wa kamati ya utekelezaji wa Ilani, tuende tukatengeneze vijitabu vidogo vidogo vya Ilani ya Mikoa, kila Mkoa uwe na Ilani yake,” amesema
Aidha, Dkt Samia ameongeza kuwa, “iseme katika ilani iliyopita tulipanga nini, tumetekeleza nini na viko wapi na ilani mpya za mikoa tumefikiria nini. Vitabu hivyo vikimalizwa kutengenezwa vitagawiwa mikoani na kila Mkoa wajue wajibu wake nini katika utekelezaji wa Ilani.”