Mwanamke mmoja nchini, Australia aitwaye Trish Webster, amefariki dunia baada kunywa dawa aina ya Ozempic kwaajili ya kupunguza kilo na tumbo iliaweze kuvaa gauni alipendalo siku ya harusi ya binti yake.
Mume wa mwanamke huyo ameeleza kuwa mkewe aliagiza dawa hizo iliziweze kumsaidia kupungua ila alijikuta akipata maradhi ya tumbo na kupelekea kukutwa na umauti “Dawa hizi hazifai kabisa” amesema mwanaume huyo.
Ozempic ni dawa iliyoidhinishwa na Utawala wa Chakula na Dawa wa Marekani kwa watu walio na kisukari cha Aina ya 2 – imekuwa ikitumiwa sana kama dawa ya kupunguza uzito duniani kote.