Walimu wakuu wawili wa Shule za Msingi Mlimani na Tunduma TC waliovuliwa vyeo vyao na kusimamishwa kazi kufuatia video ya wanafunzi wakicheza wimbo wa Zuchu wa ‘Honey’ warejeshwa kazini.

Baada ya hoja hiyo kufikishwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Spika, Dkt.Tulia Ackson aliagiza walimu hao kurudishwa kazini na kupewa nafasi ya kusikilizwa.
Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Seleman Kateti amesema kutokana na kauli ya spika, wao kama halmashauri wamelazimika kuwarudisha kazini kwa sababu taratibu hazikufuatwa.